Wazazi katika kaunti ya kisumu walikamatwa kwa kumpa mtoto wao mwenye umri wa miaka nne pombe. Wazazi hao walikamatwa baada ya majirani kulalamika kuhusu malezi ya mtoto huyo wa kiume.
Kupitia video iliyosambaa mtandaoni ambapo mvulana huyo alionekana akiwa mlevi chakari, ilionyesha mtoto huyo akilia kwa uchungu huku akijitahidi kuingia kwenye beseni ili kuoga. Mamayake alionekana amesimama kando ya mlango huku majirani wakimuuliza sababu ya kumpa mwanawe pombe.
Kitendo hicho kilizua mazungumzo na hisia tafouti kati ya watu ambapo kuna waliohisi kuwa wawili hao wanafaa kuchukuliwa hatua kali ya kisheria.
Aidha, kuna waliohisi kuwawili hao wana sababu tosha za kufanya vile ikiwemo ukosefu wa chakula ambapo wazazi hao waliamua kumnywesha pombe ili kudhibiti makali ya njaa. Wengine walihisi kuwa wanafaa kufanyiwa uchunguzi wa akili ili kupewa ushauri nasaha kwani huenda wanapitia wakati mgumu.
Mtoto huyo alinusuriwa na kupelekwa mahali salama. Wazazi hao walitiwa nguvuni na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Kondele na kushtakiwa katika korti ya Winam ambapo walishtakiwa na kosa la uzembe.
Mwandishi, Jane Mwangi.