You are currently viewing AFUENI KWA WANAKIHISTORIA

AFUENI KWA WANAKIHISTORIA

  • Post author:
  • Post category:Blog / News

Wafanyikazi wanaofanya kazi ya ujenzi katika shule ya msingi ya Voi katika kaunti ya Taita Taveta wamegundua kaburi la halaiki walipokuwa wakijenga madarasa mawili ya watoto walemavu katika shule hiyo.

Wafanyikazi hao waligundua mifupa kadhaa ya binadamu, bangili,pete na pingu kati ya uvumbuzi mwingine adimu. Kulingana na shirika lisilo la kiserikali la Urithi la Tsavo, lililothibitisha tukio hili , lilisema kuwa shule hiyo imejengwa kwenye kambi ya zamani ya wabebaji mzigo eneo la Voi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la kenya, wafanyikazi hawa walipata kaburi lililosheheni maelfu ya wanajeshi waliofariki kutokana na vita vya kwanza vya dunia mwaka wa 1914 – 1918. Ugunduzi huu ni afueni kwa wanahistoria na wanakiolojia kwani hatima yao ya utafiti kuhusu wapiganiaji na wabebaji hawa sasa imekamilika baada ya miaka mingi.

Shirika la kimataifa la Makaburi ya Vita vya Utajiri wa kawaida linalowaheshimu na kuwajali wanawake na wanaume wa jumuiya ya madola waliofariki dunia katika vita vya kwanza vya kwanza na vya pili duniani lilishukuru shirika la urithi la Tsavo kwa kuwafahamisha kuhusu tukio hilo na mambo adimu yaliyopatikana .

By Jane Mwangi