Nicholas Kiplangat ambaye ni afisa wa polisi sasa amekuwa tajiri wa milioni 11 baada ya kujishindia bahati yake kupitia mchezo wa bahati nasibu.
Akieleza jinsi aliyopata bahati ile, Nicholas alisema kuwa aliweka kiasi fulani cha pesa na kushiriki katika beti ambapo inayohusu kutoa maoni jinsi matokeo yatakavyoibuka kati ya mechi zinazocheza .Mchezo huo ambao unahifadhiwa na kampuni ya sportpesa . Nicholas alijishindia baada ya kushinda mechi 16 kati ya mechi 17.
Iwapo angeshinda mechi zote, kiplangat angejishindia milioni 291 lakini alijishindia milioni 11 baada ya kukosea mechi moja pekee. Nicholus alikuwa mwenye furaha kutokana na ushindi huo ingawa alisema kuwa angetamani sana kushinda hela zote milioni 291. Aidha, alidokeza kuwa angetumia kiwango fulani cha fedha kujenga nyumba za kupangisha katika shamba lake.
Kiplangat ambaye ni afisa wa usalama Kayole amebaki na tabasamu baada ya kujishindia hela zitakazomuimarisha kimaisha. Mchezo huu wa sportpesa umekuwa maarufu kati ya watu ambapo kuna wanaoshinda na kupata kiasi cha fedha na kuna wanaoshindwa na kupoteza pesa zao kwani mchezo huo ni bahati nasibu.
Iwapo Nicholus angeshindia hela zote milioni 291, angewekwa kwenye kumbukumbu ya historia kama washindi wakubwa kuwahi kutokea katika mchezo huo.
Mwandishi, Jane Mwangi