Mamlaka ya udhibiti wa nishati na petroli (EPRA) imetangaza bei mpya ya mafuta itakayotumiwa kuanzia tareha 15 November hadi Desemba tarehe 14.
Katika bei hiyo mpya, super petroli , diseli na mafuta ya taa zilipunguzwa kwa ksh1 hadi ksh 177 .30 , ksh 162 na ksh145. 94 kwa orodha. Hapo awali, bei ya lita moja ya petroli ya supa iliuzwa kwa ksh178, dizeli iliuzwa kwa ksh 163 huku mafuta ya taa ikiuzwa kwa ksh146. Bei ya mafuta ya taa imedumishwa kwa kiwango cha 17.68 ili kuwaepusha watumiaji kutoka kwa bei ya juu.
Katika kaunti ya Mombasa, bei ya petroli, dizeli na mafuta ya taa zitauzwa kwa ksh 174.98, ksh 159.76 na 145.79 mtawalia Mjini Nakuru itauza bei ya petroli ksh 176.62, dizeli itauzwa kwa kiwango cha ksh 161.83 huku mafuta ya taa yakiuzwa kwa bei ya 145.79.
Mjini Eldoret bei ya petroli , dizeli na mafuta ya taa zitakuwa kama ifuatavyo mtawalia ksh177.50, ksh 162.72 na ksh 146.67 . Shirika la EPRA lilisema kuwa kupunguzwa kwa bei za mafuta ni kufuatia kushuka kwa bei ya gharama ya kutwa bidhaa za mafuta zilizoagizwa kutoka nje ambayo ilishuka kwa asilimia 9.
By Jane Mwangi.