James Auta pamoja na familia yake wamebaki na huzuni na majonzi baada ya mke wake kufariki kutokana na ukosefu wa kulipa bili za hospitalini.Tukio hili lilitokea Kasuwan Magani katika eneo la serikali ya mtaa wa kajuru katika jimbo la Kaduna.
Akisimulia jinsi walivyokataliwa hospitalini kutokana na ukosefu wa fedha, James alisema kuwa alikimbia benki lakini alipata hakuwa na chochote kutokana na uhaba wa noti za Naira uliosababishwa na kubadilishwa kwa sarafu jambo lililosababisha biashara nyingi zinazohusisha ubadilishaji wa fedha kufungwa.
Kutokana na kushindwa kulipa pesa hizo, yeye pamoja na mkewe waliamua kuondoka hospitalini ingawa mkewe tayari alikuwa na maumivu. Hali ilizidi kuwa mbaya mwendo wa saa tano a usiku na James akaamua kumwita muuguzi wa eneo hilo kwani bado hakuwa na pesa za kumpeleka mkewe hospitalini.
Muuguzi huyo alijaribu jitihada zote bila kufaulu kwani marehemu alivuja damu nyingi iliyosababisha kukata roho kwake.
Mwandishi, Jane Mwangi.