You are currently viewing CHINA SQUARE YAFUNGULIWA TENA

CHINA SQUARE YAFUNGULIWA TENA

  • Post author:
  • Post category:News

Ni afueni kubwa kwa kampuni ya China square pamoja na wateja wake baada ya kufunguliwa tena kwa kampuni ile. Kulingana na kampuni hii,ilidhibitisha kuwa imerejelea shughuli zake kwazia siku ya leo Unicity kando ya barabara ya Thika.

Aidha, kulingana na ripoti ya Kenya Chinese Chamber Of Commerce [KCCC], ilisema kuwa serikali ya kenya pamoja nma jumuiya ya Wachina imeafikiana jinsi watakavyofanya biashara. Kampuni hii ambayo ilifungwa tarehe 27 mwezi februari ilifungwa kutokana na malkalamishi kuwa ilikuja kuwatoa kwenye biashara wanabiashara wadogo.Kutokana na ripoti hiyo,

kampuni hiyo ilidokeza kuwa itahakikisha kuwa imetekeleza usawa kwa wanabiashara ili kudumisha uhusiano mwema na mazingira mazuri ya kufanya biashara ili kufaidika na kuaminiana .Kutokana na taarifa ya China Square, ilisema kuwa sasa imeanza biashara.

Ujumbe huu ulidhibitishwa na kituo cha ununuzi.China square imefunguliwa rasm hii leo baada ya makubaliano kati ya serikali na wafanyibiashara wa china.

Mwandishi, Jane Mwangi