You are currently viewing HUDUMA YA PESA

HUDUMA YA PESA

  • Post author:
  • Post category:News

Mhubiri awashangaza waumini wake baada ya kufunga kufunga kanisa baada ya kupata utajiri. Kulingana na habari zilizoko, mchunganji huyo, alifunga kanisa ili kufanya biashara nyingine kwani amekuwa tajiri.

Mchungaji huyo alipata utajiri baada ya kushinda bahati nasibu ambapo alipata kiasi cha milioni 5.4 ambapo alikuwa hategemei kushinda kiasi hicho cha fedha.

Aidha, alikiri kuwa alifungua kanisa hilo kutokana na tamaa wala si kutokana na upako wa kuhubiri injili. Tukio hili limewashangaza wengi na kuibua hisia mseto kati ya waumini na wachungaji wengine.

Wengi walihisi kuwa aliwahadaa waumini ili kupata hela licha ya kupewa mamlaka ya kuwaelekeza waumini wake kwenye njia sawa, kuna waliohisi kuwa alifanya makosa kujaribu bahati yake kwani ni makosa mtumishi kucheza kamari.Aidha, waumini walihimizwa kujiepusha na wachungaji kama hao ambao wako na nia isiyo nzuri kwani kuna wengi kama mchungaji huyo.

Aidha, mchungaji huyo amesema kuwa sasa atafanya mambo mengi ambayo hakutarajia kuwa angefanya.

Mwandishi, Jane Mwangi.