Jackton Odhiambo, aliyekuwa mpenzi wa marehemu Edwin Chiloba anatarajiwa kujibu mashtaka kutokana na mauaji ya Chiloba .
Hii ni baada ya mahakama katika mji wa Eldoret kutoa amri hii. Baada ya kifo cha Chiloba, Jackton alikiri kutekeleza mauaji hayo mbele ya OCPD wa kituo cha langas akisema kuwa sababu ya kufanya kitendo hicho ni kwa kuwa Chiloba hakuwa mwaminifu.
Katika tukio hilo la mauaji, Chiloba, Jackton na mtu mwingine asiyefahamika waliondoka kuhudhuria hafla ya kufungua mwaka tarehe 31 Desemba 2022 katika klabu moja mjini Eldoret. Watatu hawa walisherekea na hata kurekodi video mtandanaoni. Baada ya hayo, kimya kilitanda kwa muda wa siku tatu ambapo mwili wa Chiloba ulipatikana Kapsiret Eldoret.
Wawili hao walikuwa wakiishi pamoja kwa muda wa mwaka mmoja kwa mujibu wa mtunzaji nyumba.Wakati huo, watuhumiwa wanne wa kesi hiyo waliwachiliwa huru baada ya mwendeshaji mashtaka katika mahakama hiyo kusema kuwa walikosa ushahidi licha ya wao kuzuiliwa siku 21.
Jackton alipelekwa kwenye mahakama ya juu ili kushtakiwa.
Mwandishi, Jane Mwangi