You are currently viewing JERAHA YAMTOA  BUKAO  SAKA UWANJANI

JERAHA YAMTOA  BUKAO  SAKA UWANJANI

  • Post author:
  • Post category:News

Nyota wa arsenali na timu ya taifa ya Uingereza Bukayo Saka alazimika kutoka uwanjani baada ya kupata jeraha alipokuwa kwenye mechi dhidi ya timu ya Nottingham forest. Saka alionekana kuhisi maumivu katika mguu wake wa kushoto walipokuwa kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo.

Mchezaji huyu alionekana akigaragara kwa maumivu yaliyotokana na kugongwa ubavu wa kulia alipokuwa akitia juhudi za kufunga bao. Kutokana na maumivu aliyopata kutokana na jeruhi hillo,alipata ugumu wa kucheza ndipo alipata matibabu kutoka kwa kikosi cha matibabu cha Arsenali kabla ya kuendelea na mchezo, aidha, dakika chache kabla ya mapumziko, maumivu yalimzidi na akalazimika kutoka uwanjani.

Reiss Nelson alichukua nafasi yake uwanjani . Bingwa huyo ambaye alivalia jezi nambari saba ni kiungo muhimu katika timu ya arsenali msimu huu huku akisaidia kikosi cha Mikel Arteta kupambana na Manchester City kileleni mwa jedwali la ligi kuu ya Uingereza. Saka amewajibika pakubwa kwenye ligi na barani Ulaya huku timu hiyo ya London ikisonga mbele kwenye timu ya Europa. Kwa sasa, timu ya Arsenali na bingwa wa Uingereza zinasubiri kwa hamu kuhusu hali ya mchezaji huyu aliyechangia katika kufunga bao la kwanza kwenye mchezo huo.

By Jane Mwangi