You are currently viewing KOCHA MKONGWE WA WAKONGWE

KOCHA MKONGWE WA WAKONGWE

  • Post author:
  • Post category:News

Beatrice Nyararia mwenye umri wa miaka 81 ni mkufunzi wa wanawake wenye umri wa miaka 55- 90 ambapo ana kikundi kiiitwacho shosho jikinge.

Alisema kuwa mradi huu ulianza mwaka wa 2007 wakati ambapo dhulma dhidi ya wanawake zilikuwa zimesheheni mtaani Korogocho. Kupitia mpango huo wa shosho jikinge, anawapa mafunzo ya ndondi ili kuweza kujikinga kutokana na wizi na dhulma zilizikithiri mtaani humo.

Nyararia alisema kuwa alipitia mafunzo ya karate kwa muda wa miezi sita kabla kuwa kiongozi wa kundi hili mwaka wa 2014. Kupitia mafunzo hayo na weledi wake, sasa amekuwa mwalimu na tegemeo kwa wanawake wenzake.

Aidha alisema kuwa kando na hayo, wanawake hao wana chama ambapo wao huchangisha shilingi 20 kila wiki . Alifafanua kuwa ingawa ni pesa kidogo, ni vigumu wao kuzipata pesa hizo kwani hawana kipato wachokitegemea kuwapa pesa hizo.Sababu kuu ya kuchangisha pesa hizo ni kusaidiana wakati wa misiba au maradhi.

Nyararia alisema kuwa ujuzi huu umemsaidia sana kwani wakati mmoja aliweza kukabiliana na mwanaume mmoja aliyejaribu kuvunja nyumba yake kwa kumdunga macho kutumia vidole vyake na kumpiga ngumi sehemu zake za siri kisa ambacho kilimfanya kuogopwa mtaani. Aidha kando na kujikikinga, alisema kuwa ndondi ni aina pia ya zoezi inayoimarisha afya kwa wanawake hasa wenye matatizo ya kimwili.

Mwandishi, Jane Mwangi