Baada ya miaka , hatimaye jengo la OTC limevuliwa neti.Jumba hili lililokuwa neti ya kijani limekuwa likitumika kama kielezo cha alipo mtu anapokuwa jijini Nairobi.
Jengo hilo ambalo limekuwa tegemeo kwa wengi hasa wageni wanaofika mjini sasa limebadilika na kubaki kawaida kama majumba mengine yaliyomo mjini Nairobi.Kulingana na ripoti, jumba hilo lilifunikwa kwa neti takriban miaka 15 baada ya kununuliwa na mfanyibiashara mmoja.Jengo hili lilisitishwa baada ya msukosuko kati ya mmiliki huyo na mmoja wa wafanyibiashara waliokuwa wamelikodisha ambao hawakutaka kuhamishwa ili kupisha ukarabati wa jengo hilo wakidai kuwa kodi yao haijakamilika.
Mzozo huo ulizidi na kesi kuwakilishwa mahakamani jambo ambalo lilifanya kujengwa kwa jengo hili kusititishwa.Kutokana na hili, jumba hili lilbaki na neti yenye rangi ya kijani kwa muda mrefu jambo ambalo liligeuka na kuwa afueni kwa wengi kwani walitumia kama kielezo cha alipo mtu anapokuwa ama anaposafiri mjini .
Kutokana na mabadiliko haya, wakenya walitoa maoni yao kupitia mtandao wa kijamii wa twitter. Baadhi yao walipendekekeza china square kukodisha jumba hilo ili kuendeleza shughuli zao.Wengi walitaka jumba hilo kupewa jina la kipekee .
Huku ujenzi wa jumba hilo ukikamilika na neti hiyo kuondolewa,wengi walisema kuwa sasa ndio muda wa wengi kupotea mjini kwani jumba la neti ya kijani walilolitegemea kwa miaka halipo tena haswaa kwa kuwa ndilo lililokuwa ishara ya alipo mtu na kuwasaidia kutafoutisha na majumba mengine.
Mwandishi, Jane Mwangi.