Waziri wa maswala ya kigeni Alfred Mutua atangaza kuwa kenya itaanza kupokea wageni mashuhuri kuanzia mwezi ujao.
Aidha, Waziri huyo alidokeza kuwa kati ya wanaotarajiwa kuzuru Nchi ya Kenya ni Jill Bidden ambaye ni mke wa Rais wa Nchi ya Marekani, Joe Biden.
Licha ya kuwa sababu yake kuzuru hazijabainika wala kufichuliwa, waziri huyo alisema kuwa Kenya ni kivutio kwa watu mashuhuri wa nchi za kigeni kutokana na msimamo wake wa kidemokrasia unaotoa mazingira yanayoheshimu haki za kibanadamu na uhuru wa kimsingi.
Aidha Mutua alisema kuwa watu mashuhuri na wengi zaidi wanatarajiwa kufika kenya miezi ijayo. Jill Bidden ambaye ni mama wa taifa wa Marekani anatarajiwa kuwasili nchini mwezi Februari.
Mwandishi, Jane Mwangi