You are currently viewing MTANDAO NI UTAJIRI

MTANDAO NI UTAJIRI

  • Post author:
  • Post category:News

Mwanasosholaiti Njoki Murira, amedokeza kuwa mtandao si wa kujivinjari na kuwafurahisha watu pekee bali pia kwani pia mtandao unaweza kukupa kipato ukiutumia vizuri. Licha ya hayo, alisema kuwa yeye ni shahidi na mmoja kati ya wanao furahia mapato ya mtandaoni kutokana na video anazozitengeneza.

Kulingana na Murira, unaweza kutengeneza video ya kujienjoy au hata kwenda live mtandaoni kulingana na unavyotaka wewe kwani uamuzi ni wako.

Njoki Murira ambaye amekuwa akiunda video katika mtandao wa tiktok ili kuwaburudisha watu mtandaoni wake kwa kunengua kiuno, amepata umaruufu na kujulikana kwenye mtandao kwa kazi yake.

Akiwajibu wafuasi wake, murira alisema kuwa ndani ya miezi mitano iliyopita, amepata zaidi ya milioni 3 kupitia mtandao wa tiktok ambazo zimemsaidia kujengea wazazi wake nyumba ya kifahari. Mwanasosholaiti huyo ambaye awali alikuwa muuzaji wa nguo za mitumba, sasa amepata utajiri kutokana na mtandao na kuboresha maisha yake.

Sasa alimewasisitiza watu kuchukulia swala la mitandao kwa uzito kwani kuna mazao mazuri.

Mwandishi, Jane Mwangi.