You are currently viewing  MTOTO ALIYETARAJIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA AJITOA HAI

 MTOTO ALIYETARAJIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA AJITOA HAI

  • Post author:
  • Post category:News

Huzuni ilitanda katika kaunti ya Kirinyanga eneo la Ndia baada ya mtoto mmoja kujitoa uhai. Mvulana huyo alikuwa anatarajiwa kujiunga na shule ya upili kidato cha kwanza baada ya mtihani wa K.C.P.E.

Huku akimwomboleza mwanawe, James Gatithi alisema kuwa tukio hilo lilitokea alipokuwa ameenda kumtafutia mwanawe shule ya upili. Alipokea taarifa za kifo cha mwanawe kupitia simu. Akisimulia zaidi , alisema ni jambo la kutamausha kwani mwanawe hakuwa na tatizo lolote walipokuwa wakizungumza.

Akidondokwa na machozi, alisema kuwa haelewi kwani waliketi na mwanawe na kukagua alichokuwa akihitaji ili kuanza maisha yake mapya ya shule ya sekondari. Shangazi yake Eunice Wanyaga alisema kuwa wna maswali mengi kwani mvulana huyo alikuwa sawa na hakuonyesha shida zozote.

Akizungumza zaidi, alisema kuwa alizungumza na marehemu na hakuskia akilalama.Alisema haelewi kilichotokea kwani wazazi wake walikuwa wakishughulikia kuhusu mahitaji yake ya shule ya kujiunga na shule ya upili.

Familia hiyo imebaki na simanzi na maswali kwani haijabaini kilichofanya mtoto wao kujitoa uhai.

MWANDISHI, JANE MWANGI