Kupitia kurasa zake za kijamii, aliyekuwa mwanahabari katika kampuni ya Royal Media services alitangaza kuhusu ujauzito wake.
Muthoni alifunga pingu yz maisha na mpenziwe Isaac Njoroge mwezi Novemba mwaka wa 2020 katika harusi ya kufana.
Aidha, alisema kuwa ni baraka kupata uja uzito huo huku akitarajia kumpokea atakaye kuwa mwanawe wa kwanza. Aliwatakia kila la heri walio katika hali kama yake na wanaojaribu ili kupata watoto.
Baada ya tangazo hili, watu tafouti kwenye mtandao walimpongeza na kumtakia kila la heri katika safari hii akiwemo dada yake.
Mwandishi, Jane Mwangi