You are currently viewing MWANA MFILISI

MWANA MFILISI

  • Post author:
  • Post category:News

Mwanamke mmoja kutoka kaunti ya Kiambu amebaki amesononeka baada ya kifilisiwa na binti yake. Akieleza yaliyojiri, Wambui alisema kuwa alielekea Nchi ya Saudi Arabia ili kupata kipato zaidi cha kujikimu pamoja na familia yake.

Alimuacha binti yake kwa jina Hottensia pamoja na ndugu yake katika kaunti ya kiambu ambapo aliwacha akiwa amewakodishia nyumba. Licha ya kuwa alikuwa mbali na wanawe, alitia bidii ili kuwakimu kimaisha. Alimtumia binti yake pesa ili awekeze kama akiba kwenye akaunti yake.

Baada ya miaka tisa, aliamua kuwacha kibarua pale Saudi Arabia ili kurejea nyumbani kwani alijua kuwa ana zaidi ya milioni mbili kwenye akaunti yake ambazo zingemuwezesha kufungua biashara. Aliporejea, alipatwa na butwaa baada ya kupata kuwa mwanawe aligeuka kuwa bwenyenye na kujitajirisha kutokana na jasho lake.Mwanawe alitumia pesa zote alizokuwa akimtumia miaka hiyo kujivinjari na kuwafurahusha wenzake kwa kupiga sherehe.

Zaidi ya yote, alichukua mkopo na kununua gari ambapo alilipa elfu 500 na kubaki na deni la elfu 750. Gari hilo licha ya kulifanya teksi, halikuwapa faida yote ila elfu 10,000 ambapo dreva alisema kuwa biashara ni mbaya. Baada ya kushindwa kulipa deni hilo, gari lilichukuliwa na kampuni.

Wambui sasa amebaki na huzuni asijue la kufanya kwani hana hata pesa za matumizi, kinachomuuma zaidi ni kutoelewa kwa nini binti yake afanye kitendo kama hicho licha ya kuwa aliwatumia pesa kila mara walipohitaji na kuhakikisha kuwa hawakosi. Licha ya kuwa Hottensia ameomba msamaha, mama yake amesema kuwa hiyo si suluhu kwani wamebaki hohehahe asijue cha kufanya kwani alitegemea kuanzisha biashara na kulipa karo kutumia pesa hizo alizomfilisi mwanawe.

Mwandishi, Jane Mwangi