Mwanaraga mzoefu Collins Injera aliyekuwa nyota wa raga atangaza kustaafu kwake. Mwanaraga huyu ambaye amecheza timu ya Kenya ya Raga amekuwa nguzo muhimu kwa timu ya wanaraga ambapo amecheza kwa muda wa miaka 17.
Nyota huyo aliweka historia mwaka wa 2016 jijini London Nchi ya Uingereza baada ya kuibuka mshindani dhidi ya Raia wa Agentina Santiago Gomez Cora na kuwa mfungaji wa miguso mingi.
Kati ya mambo muhimu ya Injera ni kushinda na kuwa mchezaji bora wa fainali baada ya kufunga mabao30- 7 dhidi ya timu ya fiji. Kupitia mtandao wake wa kijamii, Injera alisema kuwa kila kitu lazima kifikie mwisho .
Alisema mwili wake umechoka na kumuambia kuwa ni muda wake sasa kustaafu.Injera atakumbukwa kama nguzo muhimu katika kikosi cha Kenya.
Mwandishi, Jane Mwangi