Mwili wa kijana mmoja anayejulikana kama Raphael Isoe Nyamwaya mwenye umri wa miaka 25 apatikana akiwa ameiaga dunia katika nyumba ya mwendeshaji bodaboda mmoja.
Marehemu , kulingana na familia yake, alionekana akiwa hai mara ya mwisho siku ya mashujaa tarehe 20 Oktoba alipokuwa akipanda bodaboda kuelekea katika kituo cha polisi ili kuripoti kuibiwa kwa simu yake.
Raphael, aliyekuwa amehitimu na kuwa daktari wa mifugo, aliripotiwa kutoonekana na familia yake tangu siku hiyo hadi jana ambapo mwili wake ulipopatikana katika nyumba ya mwendeshaji bodaboda mmoja mwenye umri wa miaka 22. Kulingana na mke wa marehemu, alisema kuwa siku hiyo alijaribu kumpigia simu mumewe ila haikuchukuliwa na yeyote licha ya kuwa iliita. Aidha, alisema kuwa ni jambo la huzuni sana na hakutarajia kupokea habari ya kifo cha mumewe kwani ni jambo la kugadhabisha na lilimuacha na mshtuko.
Sasa muungano wa madaktari wa mifugo umetoa wito uchunguzi kufanyika wa kisa hicho kufanyika haraka huku mshukiwa wa mauaji haya akiwa ameenda mafichoni.
By Jane Mwangi.