Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 23 anashukiwa kumuua mumewe mwenye umri wa miaka 24 kwa kumdunga kisu.
Inaaminika kuwa kisa hiki kilitokea baada ya wawili hao kuwa na mzozo wa kinyumbani ambapo wawili hao walikuwa wakiishi kama mke na mume katika makazi huko Njunguini.
Inasemekena marehemu alikuwa dereva katika kampuni eneo la Arthi River kabla ya kukutana na kifo chake.
Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Arthi River Kusini Mary Njoki alisema kuwa kisa hicho kilitokea katika eneo la Njoguini ndani ya mji wa Arthi River siku ya Jumatano usiku.
Wawili hao walikuwa na mtoto mmoja mchanga aliyepelekwa katika kituo cha polisi cha Arthi River ambapo anasubiri ndugu wa wazazi .
Mshukiwa huyu amezuiliwa katika kituo cha polisi cha Arthi River amapo wahudumu wa DCI wameanza uchunguzi kuhusu kisa hicho.
Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya Shalom community.
Mwandishi, Jane Mwangi.