Rais wa Marekani Joe Biden atangaza kuwa hali imeimarika na iko huru kutokana na janga la Corona. Aidha, alidokeza kuwa japo kuna matatizo, hali bado inaimarika. Rais Joe Biden alitoa kauli hii kupitia mwongozo wa mkuu wa WHO. Tangazo hili liliwasilishwa licha ya kuwa bado watu nchini wanaaga kutokana na virusi hivyo.


Kulingana na takwimu, zaidi ya wamerikani 400 wanaathiriwa na virusi vya korona kila siku. Kufikia sasa, zaidi wa wamerikani millioni moja waeaga kutokana na virusi vya corona.Katika mahojiano na CBS, Biden alisemakuwa nchi ya Marekani inatia bidii kudhibiti virusi hivyo.
Covid 19 inaendelea kuadhiri pakubwa uchumi wa nchi ya Marekani huku Ofisi ya Kitaifa ya Utafiti wa Kiuchumi ikiripoti wiki iliyopita kuwa takriban wafanyikazi 500, 000 wamepoteza kazi zao kutokana na hali hii. Marekani imesajili idadi kubwa zaidi ya vifo kutokana na corona ikifuatiwa na India na Brazil.
Jane Mwangi, Kiambu