Mtoto mmoja afariki kutokana na ugomvi wa pakiti ya unga na mzazi wake.
Akithibitisha tukio hilo, chifu wa eneo hilo Fanuel Munanga alisema kuwa mwili wa Ezekiel Munanga ulipatikana nyumbani kwa mamake Eunice Andanje ambako ulikuwa umeanza kuoza.
Inashukiwa kuwa Andanje alimvamia mwanawe kwa kifaa butuu kilichomuua papo hapo. Andanje ambaye ni muuzaji wa chan’gaa alikuwa mlevi wakati wa tukio hilo.
Aidha , kabla ya janga hilo kutokea, walwili hao walikuwa kwenye ugomvi kuhusu pakiti kilo mbili za unga wa mahindi.Ingawa si mara ya kwanza, ugomvi wao ulikita mizizi na kusababisha kifo cha Ezekiel mwenye umri wa miaka 32.
Mwili wake uliokuwa ukiozea nyumbani ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha kakamega ukisubiri uchunguzi zaidi.
Andanje alikamatwa huku kifo cha mwanawe kikiendelea kuchunguzwa.
Mwandishi, Jane Mwangi