You are currently viewing PATRICK VIEIRA APIGWA KALAMU

PATRICK VIEIRA APIGWA KALAMU

  • Post author:
  • Post category:News

Kocha mkuu wa klabu ya Crystal Palace Patrick Vieira amepigwa kalamu baada ya kusajili mechi 12 bila ushindi wowote.Kulingana na jedwali la EPL, timu ya crystal palace inashikilia nafasi ya 12 kati ya 18 zilizopo.

Uamuzi huu ulitokana na matokeo ambayo yameshuhudiwa tangu yeye kuchaguliwa kama kocha mkuu wa timu ile. Vieira ambaye amekuwa akiwaongoza wanacrystal palace ambapo wamecheza mechi 12 mwaka wa 2023 bila ushindani wowote.

Kulinbgana na taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa palace, Steve Parish, alisema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa imefikia hatua hii lakini hawakuwa na budi kwani wanaamini kuwa mabadiliko ni muhimu na yatawasaidia katika kuinua timu hiyo haswa katika kipindi hiki ambacho wanajitahidi kuwa katika nafasi bora ili kuweza kusalia kwenye ligi kuu kwani wako kwenye hatari ya kuchujwa kutokana na matokeo duni.

Licha ya haya, Vieira mwenye asili ya Ufaransa ana historia ya ushindi alipokuwa nahodha wa timu ya Arsenal mwaka wa 2004 kwani aliwaongoza kushinda taji la mwaka huo bila kupoteza mechi yeyote.

Aidha hili ndilo taji la mwisho kushindwa na Arsenal katika EPL.Kocha huyu amepigwa kalamu baada ya miezi 18 ya utendakazi wake.

Mwandishi, Jane Mwangi.