Siku moja baada ya nchi ya Nigeria kumtangaza rais mteule, kati ya wapinzani kutoka chama cha labour, Peter Obi amepinga matokeo hayo kwa kusema kuwa uchaguzi huo haukuwa sawa na haukufanyika kwa njia ya haki na kutaka uchaguzi huo kurudiwa.
Peter Obi aliyewania kiti cha urais kupitia chama cha labour aliibuka wa tatu na katika uchaguzi kwa asilimia 37 ya kura . Kulingana na chama cha labour, uchaguzi ulisheheni makosa kama vile ubovu wa mashine na ni asilimia 28 pekee iliyoweza kupiga kura ambayo ni idadi ndogo kuliko idadi ya marais waliopita wa Nigeria.
Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja Wa Ulaya Walisema kuwa kumekuwa na upungufu katika uchaguzi na kumekuwa na ununuzi wa kura lakini ilidokeza kuwa ni mapema kusema jinsi hali hiyo ilivyoenea.
Chama cha wafanyikazi kinachoongozwa na mgombea huyo kitawasilisha pingamizi kortini ili kupinga matokeo ya urais na ushindani wa rais mteule Bola Ahmed.
Mwandishi, Jane Mwangi.