Mnamo tarehe 8 mwezi Novemba, Senegali ilipata pigo kubwa baada ya Mane kupata jeraha alipokuwa akicheza katika mechi ya Bayern Munich dhidi ya timu ya Werder Bremen. Jeraha hilo lilitokea dakika 20 tu baada ya kuanza mchezo ambalo lilimlazimu kuondolewa kwenye mchwano mzima
Mashabiki wake walishusha pumzi baada yake kujumuishwa kwenye kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 26 watakaoshiriki kwenye mchezo huo nchini Qatar.Timu ya Senegal imekumbwa na tumbo joto kutokana na jeraha la mguu la bingwa huyo kwani imesalia siku kadhaa kabla ya kombe la dunia kuanza.
Meneja wa timu hiyo Cisse amekataa kabisa kumfungia nje mchezaji huyo licha ya kukiri kuwa mechi iliyoratibiwa kuchezwa Novemba 21 dhidi ya Uholanzi itakayofungua kombe la dunia itakuwa mapema kwa Sadio kushiriki, alisema kuwa ana matumaini na timu hiyo kusonga mbele kwani hali ya Mane ni muhimu zaidi kwa timu hiyo.
By Jane Mwangi.