You are currently viewing POPO WAVAMIA KITUO CHA POLISI

POPO WAVAMIA KITUO CHA POLISI

  • Post author:
  • Post category:News

Maelfu ya popo wavamia kituo cha polisi cha Maragua huku juhudi za kuwafurusha zikigonga mwamba. Maafisa hawa walieleza hofu yao kwani wanashambuliwa na popo hawa usiku na mchana baada ya juhudi za kuwafurusha popo hawa kutumia vitoa machozi kuambulia patupu .

Juhudi za huduma kwa wanyamapori (KWS ) pia hazikufaulu jambo ambalo liliwalazimu maafisa hawa kuendelea kukerwa na popo hawa.Kulingana na maafisa , wanaamini kuwa popo hawa wanamilikiwa na wanakijiji huku wanakijiji wakiamini kuwa popo hawa wameshirikishwa na mambo ya ushirikina.

Wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa tukio hilo limeathiri pakubwa maisha yao kutokana na kelele na kunyelewa kwa nguo zao na ndege hao. Mkuu wa polisi wa Muran’ga amewashauri wakazi na maafisa kuvumilia hali hii kabla ya Shirika la Wanyamapori Kenya kutafuta suluhu.

By Jane Mwangi