You are currently viewing RAIS WA UCHINA ATEULIWA TENA KWA MARA YA TATU
Rais wa Uchina XI Jinping

RAIS WA UCHINA ATEULIWA TENA KWA MARA YA TATU

Rais wa Uchina XI Jinping anasherekea uteuzi wake wa kuwa Rais katika nchi ya Uchina kwa muhula wa tatu. Hii ni kutokana na kuidhinishwa na kura za wabunge ambao hawakupinga yeye kuwa ris kwa mara ya tatu.

Rais Xi alichaguliwa kwa kauli moja ambapo alipata kura 1,952 za wabunge.Mwanasiasa huyo aliyechaguliwa siku ya Ijumaa Machi 10, sasa ndiye atakuwa Rais aliyekaa uongozini kwa miaka mingi zaidi tangu mfumo wa kikomunisti kuanzishwa nchini humo mwaka wa 1949 kwani marais wengine nchini humo humo walihudumu kwa mihula miwili pekee.

Xi Jinping, mwenye umri wa miaka 69 amekuwa Rais tangia mwaka wa 201 3 ambapo alichaguliwa tena mwaka wa 2018 na sasa amechaguliwa tena kwa muhula wa tatu. Nguvu zake zinatokana na yeye kuwa katibu mkuu wa chama cha kikomunisti na mwenyekiti wa tume kuu ya kijeshi [CMC] .

Kutangazwa kwa waziri mkuu mpya na mawaziri wengine mbalimbali siku zijazo ni jambo muhimu na wateule hao wapya wanatarajiwa kuwa watiifu Xi Jinping

Mwandishi, Jane Mwangi.