You are currently viewing SHAMBULIO LA  AL-SHAABAB

SHAMBULIO LA  AL-SHAABAB

  • Post author:
  • Post category:News

Wanamgambo wa al- shaabab washambulia ambulensi katika kaunti ya Mandera eneo la Elwak siku ya Jumanne ilipokuwa ikisafirisha mgonjwa. Kulingana namkuu polisi wa eneo la kaskazini mashariki George Seda,tukio hili lilitendeka saa 5.50 ya jioni katika ambulensi iliyokuwa na watu wanne ikiwemo mhudumu wa afya kutoka Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Lafey, dereva, mgonjwa na jamaa wake.

Wanne hao walikuwa wakielekea katika hospitali ya Elwak walipovamiwa na watu wenye silaha. Wanamgambo hao walivuka mpaka wa Somalia na wakenya hao waliotambulikana kama Moulid Hassan aliyekuwa mgonjwa ,Hassan Shabban alkiyekuwa dereva wa ambulensi, Abdirashid Billow Hussen na Aden Dai ambao ni wahudumu wa hospitali ya Lafey.

Wanne hao, wenye asili ya kisomalia wametekwa kwa zaidi ya saa sita na hadi sasa haijulikani walipo.Maafisa wanaoshughulikia swala hili wamesema kuwa wanamatumaini kuwa wanne hao wataachiliwa.

By Jane Mwangi.