You are currently viewing SIKU ZA MWIZI

SIKU ZA MWIZI

  • Post author:
  • Post category:News

Wezi watatu wakutana na arubaini zao baada ya kukamatwa . Watatu hao walishikwa walipokuwa kwenye harakati zao za uhalifu ambapo walimpokonya mwanadada mmoja kibeti chake katika maeneo ya makongeni.

Nduru za mwanadada huyo ziliwafanya waendeshaji pikipiki katika eneo kukimbizana na jambazi hao waliokuwa wakijaribu kuhepa kutumia pikipiki waliokuwa wakitumia kutekeleza uhalifu .

Juhudi zao kutoroka ziligonga mwamba kwa wahalifu hao waliokuwa wakiendesha pikipiki kwa kasi baada ya kugongana na matatu iliyowafanya kuteleza na kuanguka. Umati wenye hasira ikiwemo wanabodaboda waliokuwa wakiwakimbiza wahalifu hao uliwakamata na kuwapiga huku wanabodaboda wakiwarushia cheche za matusi kwa kuchafulia sekta yao jina kwani walitumia bodaboda kutekeleza uhalifu.

Watatu hao waliteketezwa hadi kufa na umati wenye hasira baada ya msako mkali katika eneo hilo la Makongeni kaunti ya Kiambu.Idara ya taifa ya makosa ya jinai [DCI] ilidhibitisha tukio hilo.Aidha, polisi walipokuwasili kwenye tukio hilo watatu hao tayari walikuwa wameteketea na kuwa majivu.Walipata visu vitatu vya washukiwa,simu ya rununu,na kibeti cha mwathiriwa.

DCI hata hivyo iliwashauri wananchi kutochukua hatua mikononi mwao bali kuwapeleka washukiwa kwenye kituo cha polisi ili kukumbana na mkono wa sheria. Mabaki ya watatu hao ilipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya General Kago mjini Thika ili kutambuliwa na jamaa zao.

Mwandishi, Jane Mwangi.