You are currently viewing TABITHA KARANJA AFIKISHWA MAHAKAMANI

TABITHA KARANJA AFIKISHWA MAHAKAMANI

  • Post author:
  • Post category:News

Mkurugenzi mkuu wa keroche na seneta wa Nakuru Tabitha Karanja afikishwa mahakamani kwa madai ya kukosa kulipa ushuru wa bilioni 14.5.

Halmashauri ya ushuru nchini imeeleza mahakama kuwa hili lilitokea licha ya kuiandikia kampuni ya keroche kuwakumbusha kuhusu ulipaji wa malipo waliyofaa kulipa bado hawakutilia maanani.

Kulingana na maelezo ya KRA,kampuni ya keroche imekosa kutilia maanani maagizo yaliyotolewa na korti mwezi Julai 14, 2022 ambapo wakili wa kampuni alikuwepo.

Aidha, KRA ilitoa ushahidi wa nakala na kuziwakilisha mahakamani.Tabitha Karanja amepinga mashtaka haya na kutaka mahakama kumruhusu kusuluhisha mzozo wake na KRA nje ya korti. Licha ya ombi hili,afisa wa KRA Irene Muthee amesema kuwa hakuna stakabadhi zozote za kuonyesha kuwa wanafaa kusuluhisha nje ya mahakama.

Kampuni ya keroche imepewa muda wa siku 45 kusuluhisha mzozo huu nje ya mahakama na kama halitawezekana wataendelea na kesi ya mahakama.Kwa sasa ,KRA inataka mahakama kumhukumu mkurugenzi mkuu ambaye ni Tabitha Karanja pamoja na mkurugenzi aliye chini yake Joseph Muigai kwa kosa la kukiuka mahakama.

Hii si mara ya kwanza kampuni hii kufikishwa mbele ya korti kwa kukosa kulipa ushuru kwani awali kesi iliwasilishwa mahakamani kwa kosa hili.

Mwandishi, Jane Mwangi