Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi [INEK] Mahamud Yakubu, amemtangaza Bola Tinubu kuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais mwaka wa 2023.
Alitangaza kuwa Tinubu alizoa kura 8,794,726 zilizomfanya kushinda wapinzani wake. Tinubu, ambaye alikuwa Gavana wa zamani wa Lagos, aliwania kiti cha urais kupitia chama cha All Progressive Congres[APC] ameibuka mshindi baada ya upigaji kura nchini Nigeria uliofanyika siku ya Jumamosi.
Mwanasiasa huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 70 alishinda kwa asilimia 36 ya kura kulingana na matokeo rasmi. Mpinzani wake mkuu, Atiku Abubakar alipata kura asilimia 29 ya kura akifuatiwa na Pita Obi aliyepata asilimia 25 ya kura.
Wapinzani hao wawili walipuuzilia mbali matukio hayo wakidai kuna udanganyifu na kutaka marudio ya kura. Kupitia mtandao wa kijamii wa twitter, chama cha Tinubu kiliwashukuru WaNigeria wote kwa kumchagua Tinubu kuwa Rais. Tinubu atakabidhiwa cheti cha Rais Mteule wa Nigeria huki akimrithi Rais Muhammadu Buhari.
Mwandishi, Jane Mwangi.