You are currently viewing WANANDOA WAHUKUMIWA KWA KUSAKATA DENSI

WANANDOA WAHUKUMIWA KWA KUSAKATA DENSI

  • Post author:
  • Post category:News

Aztiazh Haqiqi mwenye umri wa miaka 21 pamoja na mpenzi wake Ammir Mohammad Ahmadi wallijipata mashakani baada ya ya kuchapisha video kwenye mitandao yao ya kijamii ya Instagram yenye wafuasi zaidi ya milioni mbili ikionyesha wakicheza densi mtaani .

Wawili hawa walipatikana na kosa la kucheza kimahaba hadharani ambapo walikuwa wakidensi, kubebana kihobela na kupiga misele barabarani kulingana na video iliyosambaa kwenye mitandao.

Aidha, wawili hawa walishtumiwa kwa ukahaba na usherati jambo ambalo sheria za kiislamu zinachukulia kwa uzito.

Kando na kupatikana na hatia ya kueneza usherati, mwanadada huyo alipatikana na kosa la kutokuwa na mavazi yanayostahili kwa wanawake kwani hakuwa amevalia buibui, vazi ambalo kila mwanamke anafaa kuvaa anapokuwa haddarani.

Kila mmoja alihukumiwa kifungo cha miaka 10 na miezi sita jela. Wawili hao walipigwa marufuku kuondoka nchini humo kwa mujibu wa Agence France Presse(AFP) na BBC.

Aidha, wawili hao pia wamepigwa marufuku kutumia mitandao ya kijamii kwa muda wa miaka miwili.

Mwandishi, Jane Mwangi.