Watalii wawili wakumbana na mauti kutokana na ajali ya barabarani walipokuwa wakizuru mbuga ya wanyama Masaai mara.
Watalii hao walifariki baada ya gari walilokuwa wakitumia katika ziara yao kukwama na kupoteza mwelekeo. Ajali hiyo ilitokea kando ya daraja la Serekani – Mara ambapo ilihusisha abiria watano ambapo watatu ni wa asili ya Ujerumani, wawili wa Uswizi.
Kulingana na afisa wa polisi, wawili walifariki huku mmoja akibaki na majeraha na kupelekwa katika hospitali jijini Nairobi ambapo alisafirishwa kutumia ndege ili apate matibabu. Wawili walinusurika bila majeraha yeyote.
Watano hao walikuwa kwenye ziara ya mbuga ya masaai mara ambayo ni moja kati ya hifadhi maarufu zinazovutia watalii nchini kenya .Aidha, pilisi wa Kenya walisema kuwa kisa hicho kinachunguzwa.
Mwandishi, Jane Mwangi